Ukristo ndio dini yenye wafuasi wengi zaidi duniani, lakini uhalisia ni kwamba kuna mashabiki wengi wa imani zaidi ya wafuasi, neno mkristo lina maana ya mfuasi wa Kristo, sasa wengi sio wafuasi ni mashabiki tu, ndani ya kitabu hiki nimekuandikia misingi iliyopo kwanza ya ukristo wenyewe lakini baadae na mkristo, hii yote ni kuhakikisha kuwa hata dini na imani zitakapochezewa kuwe na msingi unaokumbusha na kurudisha watu kwenye mstari kwa kufuata alichokisema Kristo, yapo mengi ya kujifunza unafahamu viwango vya kuamini lakini unafahamu viwango vya ukristo na namba ya uombaji wake?
Kitabu kinaelezea misingi ya imani na mfuasi wa imani ya Kikristo, ikiwa na dhana na dhamira ya wakristo kutambia kwanza misingi ya Ukristo wao wanatakiwa kuwa vipi, kutambua yapi lakini na kuyafanya yapi baada ya hapo kujitambua wenyewe kama wakristo sasa na kuitambua kwa undani imani wanayoifuata ili kujenga urafiki kati ya imani na mfuasi wa imani.
Baadhi ya mada kwenye kitabu niMaana ya mkristo: Hatua za kuamini : Mkristo ni mshindi wa kila hali: Ahadi na maisha halisi ya Mkristo : Misingi mikuu ya Ukristo hapa duniani : Maombi : Amri : Viwango vya ukristo: Hatua muhimu za kukuza imani yako: Makosa yanayofanyika na baadhi ya wakristo.
Kitabu hiki kinapatikana katika nakala aina 3.
Nakala Ngumu
Nakala Laini
Nakala ya Sauti
KUNUNUA
Upo umuhimu mkubwa wa kutambua asili zetu ili tuweze kusimama na kupata uwezo pamoja na siri zilizowekwa ndani ya asili hizo, kila mtu yuko na asili yake ambayo amezaliwa nayo sio kwa kujichagulia ama kusema kwamba ninataka kuwa na asili fulani.Zipo asili mbali mbali ambazo mtu anapozaliwa anakuwa nazo na zinamuongoza katika maisha yake hapa duniani, hapa ni baadhi yake.
1. Damu - ambayo imebeba utu wako
2. Ukoo - Imebeba tabia na mtindo wa maisha
3. Jina - Limebeba utambulisho, baraka na laana
4. Kusudi - Hii limebeba mafanikio,kipaji, baraka na ukuu wako
uhalisia ni kwamba asili yako haipotei kwa kutokuifahamu watu wengi wametekwa na asili zao na wao wanahisi ni mazoea au ndivyo ilivyo, maana ya ukristo haikuwa kuitengua asili ila kuikamisha kwa amri kuu ya UPENDO, ndani ya kitabu hiki utajifunza kwanini asili yako ni muhimu katika mafanikio yako lakini kwanini unatakiwa kujitambua kiasili wewe ni nani? Ili kujua kusudi lako ni lazima ujitambue.
Nakala Ngumu
Nakala Laini
Nakala ya Sauti
KUNUNUA
Moja kati ya maeneo yanayowaangusha vijana wengi sasa hivi, kesi za mahusiano ni nyingi sana lakini ukiangalia mzizi ni wivu na maarifa machache kuhusu mahusiano, hii ndio sababu ya kuandika kitabu cha saikolojia ya mahusiano, ili kutoa elimu ya ufahamu kuhusu mahusiano lakini ustawi wake, hiki sio kitabu cha mapenzi ila ni kitabu cha mahusiano ndani yake kimegusa kila nyanja ya mahusiano ili kumsaidia msomaji kutambua njia sahihi zaidi kwake kupita
Mahusiano ni jambo muhimu sana kwenye maisha yetu, mafanikio yetu yamefichwa kwenye mahusiano yetu, ukiwa na mahusiano mazuri na watu ni rahisi sana kufanikiwa lakini sio mahusiano na watu hata ukiwa na mahusiano mazuri na pesa zako utafanikiwa kwa urahisi sana, hivyo kutambua saikolojia ya mahusiano ni jambo la msingi katika maisha yetu ya kawaida lakini hata kwenye mahusiano ya mapenzi pia bila kujua saikolojia yake hauwezi kudumu kwenye mahusiano yako.
Kitabu hiki kitakusaidia kwanza kuyaelewa mahusiano lakini pia kutambua mbinu za kuyasimamia na saikolojia ya kuyatunza.
Nakala Ngumu
Nakala Laini
Nakala ya Sauti
KUNUNUA
Biashara ndio uti wa mgongo wa uchumi. maarifa yake ni muhimu kwa ustawi wa uchumi wa mtu na taifa, ndani ya kitabu hiki kuna page 242 za maarifa. Humu ndani kuna maarifa kuhusu kujitambua kiasili,kwa nyanja zote ikiwemo kibiashara lakini jinsi ya kupata wazo bora na kulisimamia kitabu hiki kinakupa mwongozo wa kuanza na kuendeleza biashara yako hasa kwa mpango endelevu wa kizazi chako na cha baadae.
Tukianza kugusia mafanikio ya kiuchumi hauwezi kuacha suala la biashara, biashara kwenye uchumi ni kama maji kwenye mwili wa binadamu, mtindo ama utaratibu wa kupata pesa na kukuza uchumi umewekwa chini ya kivuli cha biashara haijalishi ni katika mtindo gani huduma au bidhaa bado zote ni biashara.
Hivyo elimu ya biashara ni muhimu sana kuitambua kwanza wewe na baadae kizazi chako, mafanikio halisi yako kwenye biashara, hata kama umeajiriwa sehemu tambua kuwa kwa bosi wako wewe ni sehemu ya biashara yake ambapo unaifanikisha kwa namna moja ama nyingine, ndani ya kitabu hiki nimekuwekea mwongozo bora wa biashara ambapo inaanzia hatua ya chini kabisa kwenye wazo hadi kuanzisha biashara na kisha kuiendeleza.
JIPATIE NAKALA YAKO SASA
Nakala Ngumu
Nakala Laini
Nakala ya Sauti
KUNUNUA
Kwa maulizo ama uhitaji wowote wasiliana nasi