Echu Academy ni mahali ambapo utapata elimu ya maisha ambayo inaunganisha uwazi uliopo kati ya elimu ya darasani na elimu ya mtaani ( Maisha), watu wengi wanafeli kwenye maisha kwa sababu ya kutumia elimu ya darasani peke yake ambayo inakuandaa kufanyia kazi maarifa pindi ambapo vitu vikiwa tayari lakini elimu ya mtaani yenyewe inakutaka kuanza kutengeneza kitu na kukisimamia kabla ya kufanikiwa, hivyo kuna misingi mingi na elimu nyingi muhimu ambayo inakosekana na kufanya kundi kubwa la wasomi kufeli lakini pia kundi kubwa la wasio kuwa wasomi kujiona hawafai
Echu Academy ndio suluhisho kwa watu wote wawili hawa na watatu ambae anatamani kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mambo yakadhihirika, unahitaji zaidi ya elimu moja kufanikiwa jambo lako, kupitia Echu Academy utajifunza jinsi ya kufanya mambo kwa kufuata kanuni ya mtaa na kanuni za weledi.
Kupitia Echu Academy utajifunza kozi mbalimbali ikiwemo mafanikio yako ya
1. Kimwili
2. Kiafya
3. Kiakili
Bila ya kuwa na utimamu wa hivi vitu vitatu basi uwezo wako wa kuamua na kutenda unakuwa umeathirika na udhaifu wa eneo moja ama jingine hivyo kozi zetu zitalenga kukuimarisha maeneo yote kwa ajili ya kutengeneza mafanikio yako kwa uhakika.
Karibu Echu Academy ujifunze na kupata maarifa yatakayo kusaidia kuishi na kufanikiwa mtaani, elimu yetu ni maarifa na sio kutoa cheti, hivyo unaposoma zingatia maarifa zaidi ya cheti, sisi tunaamini cheti halisi kinatolewa mtaani na mafanikio yako ama kufeli kwako. Huko ndio kuna viwango sahihi vya ufaulu na ufanikishaji.
Echu Academy - Maarifa yenye maarifa.
Kwa maulizo ama uhitaji wowote wasiliana nasi