Wajasiriamali lift up kama jina linavyojieleza lenyewe huu ni mradi wa kumsaidia mjasiriamali kuweza kufanya biashara yake kwa ubora zaidi, ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa kuna ushindani mkubwa sokoni hasa upande wa kujitangaza na kujenga chapa, lakini gharama za kufanya zote hizo kwa pamoja zimekuwa changamoto kubwa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo, hapo ndipo Wajasiriamali lift up inapofanyika msaada kwako.
Ni huduma ya kumnyanyua mfanyabiashara, kutoka kwenye wazo kutoka kwenye bidhaa hadi wateja na soko lake, (Biashara nyingi zinafeli sababu ya soko sio bidhaa/huduma
WALENGWA
Watu wenye biashara ama mawazo lakini hawajui jinsi ya kufanya au hawana mipango na mbinu nzuri za kutangaza na kurasmisha.
HUDUMA TUNAZOTOA
1. Kuhakikisha wazo la biashara na mlengo wa soko kwa kuangalia fursa na uhitaji
2. Kutengeneza mpango biashara
3. Kusajili kampuni ( Jina la biashara)
4. Kutengeneza nembo ( Logo)
5. Kudizaini na kuprint vitu vya kurasmisha biashara kutoa huduma ( Risiti, business cards,letterhead etc)
6. Kutengeneza akaunti ya biashara mtandaoni
7. Kuisimamia akaunti za biashara mtandaoni
8. Kuunganisha akaunti ya biashara na huduma ya Sponsored Ads
9. Kudizaini matangazo ya mtandaoni ( Online Ads)
10. Branding ya biashara.
Huduma hizi zinatolewa kwa mkopo kwa kutegemea na aina ya biashara ama wazo, ambapo tutakuhudumia taratibu zote kwa nusu bei ya mchakato wote na kisha malipo yanayosalia utaanza kuyalipa baada ya miezi 3 ndani ya kipindi cha miezi 6.
- UNA WAZO LAKINI HUJUI UTALIFIKISHAJE SOKONI
- UNA BIDHAA LAKINI UKUAJI WAKE NI MGUMU?
- UNA BIASHARA LAKINI HAIFANYI VIZURI MTANDAONI
Karibu Wajasiriamali Lift Up.
Kwa maulizo ama uhitaji wowote wasiliana nasi