ECHU TUONGEE FAMILIA

  • UTANGULIZI
  • HUDUMA
  • TUNAFANYAJE

Familia ni taasisi ya kwanza kutengenezwa na Mungu mwenyewe ikiwa na dhamira na lengo la kuijaza dunia lakini kuistawisha na kufanya kuwa mahali salama sana na penye amani,lakini kutokana na maendeleo na utandawazi pamoja na vile tunavyoviita uvumbuzi kuna mambo mengi ambayo yameharibika kutoka kwenye taasisi hii ya kwanza.

1. Mmomonyoko wa maadili

2. Mawasiliano hafifu ndani ya familia

3. Pamoja bila umoja

4. Uchumi wa familia kudorora

5. Asili kupuuzwa na utandawazo kuheshimiwa zaidi

Hapo juu ni mifano michache ya baadhi ya matokeo ya kukosa uimara wa taasisi hii ya familia, nahapo ndipo tulipoanzisha mradi wa Echu tuongee familia maalum kwa ajili ya familia kujenga na kurudisha mahusiano na kujenga mafanikio ya pamoja.

Huduma ya Echu Tuongee Familia ina maono ya kurudisha misingi ya familia na kutengeneza muunganiko chanya, ambao utaondoa daraja kati ya wanafamilia hasa upande wa mawasiliano, malengo na uchumi. Lugha na mlengo wa familia nyingi ni tofauti na uhalisia, utakuta baba anamawazo tofauti na mtoto, baba anawaza mtoto awe Dokta na mtoto anawaza kuwa mwanasheria, mwisho wa siku kama hakuna mawasiliano mazuri hakutakuwa na malengo ya pamoja na mawasiliano pia yanaharibika kunakuwa na daraja.

Kupitia Echu Tuongee familia, tunatengeneza munganiko wa mawasiliano kati ya familia kwa nyanja zote, wanafamilia watapata nafasi ya kutengeneza munganiko, mtoto atapata nafasi ya kutoa maoni na mawazo yake yatamfikia mzazi, mzazi atatambua mawazo ya mtoto, lakini pia atapata nafasi ya kutoa mawazo yako na maoni kabla ya kufahamu mtoto aliwaza nini, ili familia ifanikiwe ni jambo la msingi sana kuwa na muunganiko sadifu ambao utatengeneza malengo chanya kwa familia. Kiroho, kiuchumi na kijamii.

Hivyo kupitia Echu Tuongee familia, tutaondoa daraja la mawasiliano kati ya mzazi na mtoto, familia nyingi zinaishi pamoja lakini sio kwa umoja, Echu Tuongee Familia tuko hapa kwa ajili ya kuondoa tabaka hilo na kuleta muunganiko chanya.

Wasiliana nasi leo ili kuweza kupata huduma hii itakayokuwa mhimili wa mafanikio ya famillia yako na kizazi chako.

Wasiliana nasi leo

Kwa maulizo ama uhitaji wowote wasiliana nasi

Whatsapp